Na SMAUJATA habari
KATAVI
26 October 2024.
Viongozi SMAUJATA wa mkoa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti mkoa Shujaa Razack Salim,Katibu SMAUJATA mkoa Shujaa Edward Nswima wakiambatana na Viongozi wa Wilaya ya Mpanda Mwenyekiti Shujaa Dachi Dades,katibu shujaa Othmani Mbarouk wamefanya Mazungumzo ya kina na kiongozi wa kitaifa Shujaa PROTAS PETER TENDWA Mkurugenzi wa kamisheni na Utawala Taifa kuhusu uratibu wa shughuli za SMAUJATA mkoa wa katavi na kuisaidia jamii kuhusu masuala ya ustawi na maendeleo.
Aidha kiongozi huyo kutoka Taifa ameishukuru idara ya ustawi na maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi kwa ushirikiano wao kwa mashujaa wa SMAUJATA mkoa kwa kuendelea kutoa muda wao kwa viongozi hao katika kuitumikia jamii ya wana Katavi. Pia amesisitiza ushirikiano na nidhamu kwa viongozi wote na kuendelea kufuata utaratibu wa kimajukumu ili kufanikisha shughuli za SMAUJATA kwa mkoa wa Katavi kwa maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla.
Shujaa PROTAS TENDWA aliwasilisha salamu za Mwenyekiti Taifa kwa Mashujaa wa mkoa wa Katavi.