NA SMAUJATA LIWALE – LINDI
Aprili 03,2015

Katika jitihada za kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii, Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Wilaya ya Liwale imekutana na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Bw. Namaleche, kwa lengo la kujitambulisha na kujadili ushirikiano wa pamoja.
Bw. Namaleche aliwapokea kwa moyo mkunjufu na kuwahimiza kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na masuala mengine ya haki za binadamu. Ushirikiano huu unalenga kuleta uhamasishaji mkubwa kuelekea tukio la Mwenge wa Uhuru utakapowasili katika Wilaya ya Liwale.
SMAUJATA imeahidi kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi kuhusu haki, usawa, na ustawi wa jamii.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa SMAUJATA kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ukatili na hatua za kuchukua ili kulinda haki za kila mmoja katika jamii.
Imeandaliwa na Afisa Teknolojia na Mifumo SMAUJATA Wilaya ya Liwale.
Ndg: Yazidu Nassoro



