
Na Smaujata Manyara
10/4/2025
Mwenyekiti wa Smaujata Manyara Shujaa PHILIPO SANKA ameshirikiana na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa na Mkuu wa wa Dawati La Jinsia Mkoa wa Manyara,Polisi Kata kata ya Babati na Afisa ustawi halmashauri ya Mji Kutoa Elimu ya Ukatili wa Kijinsia kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Angoni

Aidha Amewasihi wanafunzi kuendelea kua mstari wa kwanza kujilinda dhidi ya Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili kuzuia na inapobainika Matukio yaripotiwe maeneo yote yaliyoainishwa kisheria

Mwisho amewataka wanafunzi wanapoenda likizo kuendelea kusoma kwa Bidii na kuepuka kuchangamana na Makundi yasiyo na maadili kwenye Jamii.
