Na SMAUJATA Habari
12.04.2025

Theme:Strengthening Mult-Stakeholder Collaboration in GBV Response.
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu, GH FOUNDATION na Uongozi wa SMAUJATA Taifa kunichagua kuwa mwakilishi katika mafunzo haya muhimu yaliyofanyika leo trh 12.04.2025 kuanzia saa 3:30 asubuhi – 10:30 jioni.
Napenda kuwashirikisha baadhi ya mambo ya msingi yaliyoongelewa kwa kina na kusisitizwa katika mafunzo haya:
Mafunzo yalianza kwa kuelezea kidogo kuhusu GH FOUNDTION kuwa ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha hasa na kupambana na Magonjwa yasiyo ambukiza na kupambana na Ukatili wa kijinsia na kwamba wamefanikiwa kuigusa jamii kwa namna mbalimbali katika maeneo hayo na wanaendelea kutoa huduma ikiwemo kutoa elimu, vifaa tiba na misaada mbalimbali kwa wahanga wa Ukatili wa Kijinsia hasa kwa Watoto wakishirikiana kwa karibu sana na Serikali ya Tanzania(Muhimbili Hospital, Mwananyamala Hospital n.k).
Baada ya hapo Mwezeshaji wa kwanza(Wakili Msomi Maduhu) aliongelea namna mbalimbali zinazotumika kupambana na Ukatili kwa kutumia Sheria zetu na jinsi zinavyosaidia kwa kiasi kikubwa kutoa haki kwa wahanga wa ukatili hasa watoto na wanawake lakini alisisitiza swala la wadau wote kutambua na kuanza kusisitiza uwepo wa MFUKO WA FIDIA kwa case zote za Ukatili ili baada ya ushahidi kutolewa na hukumu kutolewa kwa wahusika basi wahanga wapewe fidia.(Swala hili lilipendekezwa na Msekwa 1979 na limeendelea kuzungumziwa na wadau lakini bado halijtungiwa sheria na kuhakikisha mfuko huo wa fidia upo na unafanya kazi kisheria)
Hivyo wadau na Serikali tunawajibika kuliangalia hilo na kuhakikisha linafanyiwa kazi kwa umuhimu wake.

Pamoja na hayo aliongelea pia kuhusu namna ambavyo vitendo vya ukatili vingi au case nyingi za ukatili zinawakuta watoto(43% ya kesi za ukatili ni za watoto) na ma-Afisa Ustawi wanahusika moja kwa moja kusimamia Case hizi kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hili liliongelewa kwa kusisitiza pia uwepo wa Ma-Afisa ustawi kuanzia ngazi ya Kijiji maana kwa sasa wapo kuanzia ngazi ya KATA.
Eidha changamoto nyingi zinazofifiza haki kutolewa katika kesi za ukatili zilitajwa kadhaa ikiwemo:
-Kucheleweshwa kwa taarifa za ukatili
-Uzembe wa baadhi ya waendesha mashtaka.
-Ukosefu/Uhaba wa mafungu ya pesa za kufatili vitendo vya ukatili hasa katika ofisi za Polisi na Ustawi wa jamii ambao ndio watendaji wa karibu zaidi na jamii.
-Ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara ya aina za ukatili wa kijinsia na namna ya kuzifnyia kazi.
-Mapungufu ya Ushahidi.
-Ndugu kufichiana siri na kutokutoa ushahidi(Ukatili mwingi unafanyika majumbani)
-Majaribio ya kufubaza kesi. Ndugu kujafiriana na kumaliza kesi nje ya mifumo ya sheria. n.k
Pamoja na hayo…kutokana na baadhi ya wajumbe kulalamikia swala la washtakiwa wa vitendo vya ukatili kuonekana mitaani,Wakili alijaribu kueleza namna ambavyo sheria zimetoa nafasi za udhamini wakati kesi zinaendelea kabla ya hukumu na alibainisha baadhi ya makosa yasiyo na dhamana kama ifuatavyo
^Kesi za mauaji
^Rushwa
^Uhujumu Uchumi
^Ufisadi
^Ugaidi n.k
Mwezeshaji wa pili alikuwa Dr.Chris Mauki ambae alielezea namna Ukatili mwingi unavyosababishwa na matatizo ya Kisaikolojia na kufafanua aina kadhaa za vyanzo vya ukatili ikiwemo ukatili wa maneno, aliongeza kuwa wanawake wengi wanafanyiwa ukatili na wanaume kwa sababu ya kuwaumiza wanaume Kisaikolojia kwa muda mrefu na kwa sababu mazingira na Asili ya mwanaume sio kuongea yanayomkabili basi anapozidiwa anafanya ukatili kwa mwanamke na matokeo yake anaishia matatani ikiwemo kufungwa n.k hivyo wadau tunapaswa kuwa makini na namna tunavyoumiza hisia au saikolojia za wanaume,lakini pia wanawake na watoto maana historia inqonyesha watenda ukatili wengi ni wahanga wa ukatili au wamewahi nao hufanyiwa ukatili kwa namna moja au nyingine, lakini pia imesisitizwa wazazi kuwapa muda watoto na kuwasikiliza ili kutambua ukatili wanaotendewa lakini pia kujitahidi kuwapa elimu mapema ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili.
Pia alitoa angalizo kuwa vipo vitendo vingi vya ukatili ambavyo havina ushahidi hivyonavyo vitafutiwe sheria au tiba thabiti maana ni vingi mnooo ikiwemo watoto
~kushikwashikwa sehemu zao zasiri
~kulazimishwa kunyonya sehemu za siri za hao watenda ukatili
~Kuingiziwa vidole
~kutishiwa n.k

Lakini pia washiriki wote tulipata nafasi ya kujadiri na kuwasilisha mambo matatu
1.UMUHIMU WA KUKUSANYA TAARIFA ZA UKATILI ….(Kwanini tukusanye Taarifa za Vitendo vya Ukatili)
-Kwa ajili ya kufanya tathmini
-lli kupata Takimu
-Ili kuwabainisha waharifu
-Ili kufahamu mbinu wanazotumia waharifu
-Ili kubuni mbinu mpya za kupmbana na Uharifu
-Ili kufahamu rika gani wanaathirika zaidi, Maeneo gani zaii,jinsia gani zaidi n.k.?
-Ili kupanga mikakati zaidi katika kutatua tatizo na kuangalia uwezekano wa kutunga sera/Sheria ili kutokomeza tatizo.
2.KITU GANI CHA KUZINGATIA ILI KUWA NA TAARIFA SAHIHI.
-Usiri wa Watoa huduma.
-Utayari wa wahanga katika kutoa taarifa za vitendo vya ukatili walivyo/wanavyotendewa
– Chain au utaratibu na ngazi za utoaji taarifa zifahamike vizuri kwa watoa huduma na jamii kwa ujumla…mfano…Serikali za mitaa,Dawati,Polisi n.k na taarifa zinapoletwa ziwe kamirifu mfano kama muhanga ni wa kike au kiume, Umri wake, Kundi alilopo…mtoto, mzee, mlemavu n.k
3.MIFUMO GANI ITUMIKE KUKUSANYA TAARIFA.?
-Namba ya bure 116
-Kamati zilizowekwa ziboreshwe kuanzia ngazi ya kijiji.
-Ushirikishwaji wa wanawake na uhamasishwaji katika kukomeha hili
-Ushirikishwaji wa jamii nzima.
-n.k
Eidha pamoja na mambo mengine mengi yaliyozungumziwa Viongozi wa dini wamesisitizwa kwa mapana na marefu kuacha kurahisisha kesi za Ukatili kwa kuwaombea tuu mtenda na mtendewa na kuwaambia wasamehe 7×70 kama biblia inavyosema badala yake wafatilie kwa makini na kuwashirikosha vyombo mbalimbali vinavyohusika na maswala ya kesi za ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kesi zinafanyiwa kazi kwa ufasaha na umakini hii itapunguza mauaji yanayoendelea hasa ya anandoa.
Pia washiriki wote tulisisitizwa kuhakikisha una taarifa kamili za vitendo vya ukatili na kufatilia kesi mwanzo mpaka mwisho unapoletewa kesi hizo usiache njiani hakikisha haki zinatendeka na muhanga anapata haki yake.
Kwa haya machache naomba kuwasilisha:
HERIETH GADSON BALAGAYE +255717123432, Social Worker, Mama wa watoto wengi.Human Dignity Tanzania(Mkurugenzi Idara ya Kurugenzi Ustawi wa Jamii, SMAUJATA )
12.04.2025