Na SMAUJATA – Dar es salaam,
April 13/2025

Uongozi wa Smaujata mkoa wa Dar es salaam, ukiongozwa na Shujaa Mary Mwangaba;katibu na Shujaa huki katibu hamasa mkoa, tukishirikiana na maafsa ustawi wa mkoa wa Dar es salaam kata ya Kigogo, tumefanikiwa kumfuatilia mtoto aliekua ametelekezwa na mama yake kijijini mkoa wa Tanga, Handeni kwa bibi yake, ambae Hana uwezo wowote na bila matunzo yoyote , ambapo ilimsababishia mtoto kushindwa kuhudhulia shule Kila mara kwa kukosa mahitaji muhimu kama chakula na kumlazimu kufanya kazi mitaani ili apate kula na kushindwa kwenda shule,
Tulipo pata taarifa kutoka kwa shujaa ndipo tulipoanza kumfuatilia na kugundua tukaamua kutafuta namna ya kumsaidia mtoto ili awe sehemu salama aweze kuendelea na masomo yake,
Tunashukuru ushirikiano tulio upata toka kwa baba wa mtoto , bibi, dawati , na maafsa ustawi, walimu wa shule aliyokua anasoma, Sasa mtoto Yuko dar kwa baba yake na ameshaanza shule.
Hekima na umoja ushindi na ushujaa Smaujata
Imetolewa na katibu mkoa wa Dar es salaam
Shujaa Mary mwangaba