Kuhusu SMAUJATA

SMAUJATA ni Jumuiya ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto nchini Tanzania iliyoanzishwa na Sospeter Mosewe Bulugu mwaka 2022 chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu. Jumuiya hii hulenga kupinga kila aina ya ukatili, ukiwemo ukatili dhidi ya watoto.

Smaujata inafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za serikali zinazohusika katika kutoa haki, ambazo ni ofisi za Ustawi wa Jamii, polisi pamoja na Takukuru, hasa upande wa rushwa ya ngono.