Na SMAUJATA HABARI MWANZA
03/04/2025

Wanawake na Wasichana SMAUJATA Mkoa Wa Mwanza Wamekuja na Mbinu Mpya katika Kujikwamua Kiuchumi Ikiwa Na Lengo la Kuzitumia Fursa zinazotelewa Kwa Sasa na Serikali ya Awamu ya Sita Inayo Ongozwa na Jemedari Rais Samia Suluhu Hassan.
Moja kati ya Mipango walio kuja Nayo ni kuanzisha Kikundi Kidogo Cha wajasiliamali Ambapo katika Kikundi hicho watajifunza Utengenezaji wa Sabuni, Batiki, Shampoo ,Na Mengine Mengi Huku wakiweka Mbele Kipaumbele Cha Utengenezaji wa Sabuni na Batiki.
Kikao Hicho kilicho ongozwa na Makam Mwenyekiti SMAUJATA Mkoa wa Mwanza Shujaa Agripiner Faustine Mussita Amewasisitiza Wanawake wa SMAUJATA MWANZA Kujitokeza Kwa Wingi Kushiriki katika Miradi Hii Midogo midogo Kwani Kwa Asilimia Kubwa Inalenga Kumjengea Uwezo binafsi Mtu Mmoja Mmoja Kupitia Madarasa Kwa Vitendo yanayo husu ujasiliamali.

Aidha Naibu Katibu wa SMAUJATA MWANZA Shujaa Godfrey Julius Amewasisitiza Mashujaa Wa SMAUJATA kujisajili y Kwa Wingi na kulipia Ada Ya Mwanajumuhiya Ikiwa Jumla Ni Tsh 15,000/= Na Inalipwa Kwa Lipa Namba ya Tigo (Yas) 19603878 Au Unaweza Kuwasiliana Na Kiongozi wa SMAUJATA katika Eneo lako Kwa Msaada Zaidi.

Huku Shujaa Hakim Abdul Katibu SMAUJATA Mkoa Mwanza Amesisitiza Mashujaa Kuvitumia Ipasavyo Vitambulisho hivyo visije vikatumika Tofauti na Malengo Kusudiwa. “Tunapambana na vitendo vya ukatili katika Jamii, Tusije Tukatoka Kwenye Malengo yalio Tukusanisha Hapa, Malengo yalio Tukusanisha Hapa ni Kuisaidia Serikali kupambana na Vitendo Vya Ukatili, Mimi Ninaamini waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili ni Wanawake na Watoto, Sisi wenyewe tuhakikishe lengo la SMAUJATA linatimia” Ameyasema hayo Alipo Pewa nafasi ya Kuzungumza Katika Kikao hicho.

Kataa Ukatili Wewe Ni Shujaa
✍🏻 Imeandikwa na Philimon Robert



