SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII TANZANIA
HEKIMA NA UMOJA, USHINDI NA USHUJAA SMAUJATA
Jiunge na Mashujaa wengine Hapa
Kuhusu SMAUJATA
SMAUJATA ni jumuiya ya kijamii ambayo imesajiliwa chini ya sheria ya asasi za kiraia (CAP .337 RE 2022) kwa usajili namba S.A.23969, SMAUJATA ilianzishwa na shujaa Sospeter Mosewe Bulugu mwaka 2022 kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya na kuleta maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi.
Dira ya SMAUJATA
Dira ya SMAUJATA ni kuwa na Taifa lenye kizazi huru chenye Haki na Usawa Kitakachoweza Kujitegemea na Kuzitambua na kutumia Ujuzi, Maarifa na Vipaji katika kujenga jamii yenye Maendeleo Endelevu
Dhamira Ya SMAUJATA
Dhamira Ya SMAUJATA ni Kuiwezesha na Kuijengea Jamii uwezo wa kutambua na kuiishi Misingi ya Haki na Usawa ili kutumia ujuzi, maarifa na vipaji katika kujenga jamii yenye Maendeleo Endelevu.
Imani Yetu Mashujaa
Imani ya SMAUJATA ni “HEKIMA NA UMOJA“, “USHINDI NA USHUJAA SMAUJATA“
Malengo Ya SMAUJATA
i. Kushirikiana na wanajumuiya katika kuainisha fursa na changamoto zinazowakabili Pamoja na kuwaunganisha na jamii katika kuwawezesha kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa ya sera za kisekta na mikakati yake kuinua ustawi wao na wa jamii.
ii. Kuelimisha kuelimisha wana jumuiya na jamii kuondokana na fikra, imani, mila, desturi na tamaduni zinazokinzana na maendeleo kwa kutumia semina, sanaa, warsha, makongamano, vyombo vya habari, matembezi ya amani, vipeperushi kuhusu haki, usawa, fursa na sera mbadala kwa maendeleo endelevu na kuiwezesha jamii kutekeleza haki na malezi ya mtoto.
iii. Kuratibu utekelezaji na uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika programu na mipango ya maendeleo ya wana jumuiya na jamii nzima katika sekta mbalimbali.
iv. Kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji vya wana jumuiya katika ujuzi, utaalamu na ubunifu ili kujenga jumuiya yenye uwezo wa kujitegemea.
v. Kushirikisha wana jumuiya, kushirikiana na serikali, wananchi na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika shughuli za utoaji wa elimu na fursa za maendeleo na majanga katika jamii pamoja na kubadilishana mawazo, maoni na mbinu wezeshi ili kuishauri jamii na serikali katika kuboresha na kufanikisha vipaumbele vya ustawi na maendeleo ya jamii.
vi. Kufanya shughuli zingine zozote zinazohusu maendeleo na ustawi wa wana jumuiya na jamii kwa ujumla.
Dhana Ya Jumuiya Ya SMAUJATA
Dhana ya Jumuiya ya SMAUJATA ipo katika kupinga vikali, Kuibua na Kutokomeza aina zote za matukio au vitendo vya ukatili katika makundi mbali mbali ya jamii kupitia wananchi wazalendo na wadau mbali mbali kushiriki moja kwa moja katika maeneo yao dhidi ya vitendo hivi viovu
Kauli mbiu ya jumuiya hii imelenga kuhamasisha wananchi kila mmoja kushiriki kufanya yafuatayo:-
- KUELIMIKA na kuelimisha wengine kuhusiana na masuala yanayohusu ukatili ikiwa pamoja na kufahamu aina za ukatili madhara yake, hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivi na kufahamu ushiriki wa wananchi katika hili.
- KUWA MUANGALIZI WA JAMII na kuchukua hatua kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili.
- KUSHAURI asas, wadau wa maendeleo, jamii, serikali na vyombo mbali mbali vya maamuzi katika kufanya maboresho mbali mbali ya huduma za kijamii hasa zile ambazo zikiwa hafifu zinaweza kuchochea vitendo vya kikatili
Fahamu Zaidi Kuhusu SMAUJATA
SMAUJATA ilizinduliwa rasmi mnamo Juni 16, 2022 na Mh Dorothy Gwajima (Mb) – Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa Jijini Dodoma.
SMAUJATA ni kifupi cha maneno Shujaa Wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania.
SMAUJATA inaendesha kampeni huru ya kitaifa ya wananchi wazalendo wanao jitolea kuibua, kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili ambapo kufikia Septemba 2024 Jumla ya Watanzania 10,675 katika Mikoa yote nchini wamejiunga na Jumuiya hii.
TAARIFA
Habari Muhimu
See MoreHabari Mpya
UONGOZI WA SMAUJATA
Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu
Mwasisi na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya
Shujaa Simon Ikumbo
Katibu Wa Seneti
Shujaa Winifrida Mahenye
Mkurugenzi wa Kamisheni na Utawala
Shujaa Gaudence Mnyang'ali
Mkurugenzi wa kamisheni na Utawala
Shujaa Protas Tendwa
Mkurugenzi wa kamisheni na Utawala
Shujaa Dr Magolanga Shagembe
Mkurugenzi Maendeleo Saikolojia, Jinsia na Makundi Maalumu
Shujaa Nanyorry Mwasha
Mkurugenzi wa wanachama, Uhusiano na Mahusiano ya Kimataifa
Sospeter Mosewe Bulugu
Mwasisi na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya
Add Your Heading Text Here
Add Your Heading Text Here
Add Your Heading Text Here
MAONI YA WADAU
“Utoto wangu ulijaa unyanyasaji, kuniacha nikijihisi nimevunjika na peke yangu. Kiwewe kilionekana hakiwezi kushindika, lakini kwa msaada sahihi, nilipata nguvu ya kukishinda
“Nikiwa nakua, nilipitia unyanyasaji mkali wa kimwili na kihisia. Ulinivunja moyo na kunifanya nijihisi sina thamani. Lakini nilipofikia hatua ya kuomba msaada, nilipata mtandao wa msaada uliobadili maisha yangu.
MASWALI YA YAULIZWAYO MARA KWA MARA
Hujumlisha Hatua za ulinzi kama vile amri za zuio, Kuondolewa kutoka mazingira mabaya yenye kuchochea unyanyasaji.
Matokeo yanaweza kujumuisha mashtaka ya jinai, kifungo, na kupoteza haki za mzazi. Ukali hutegemea aina na kiwango cha unyanyasaji.